October 5, 2018


DULLA


Baada ya kukwepana kwa muda mrefu, hatimaye siku imefika ambapo Francis Cheka anatarajiwa kupambana na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ katika pambano la uzito wa kati kuwania mkanda wa Super Middle Weight la raundi 12 ambalo limepewa jina la Nani Mfalme? (Who is King?) litakalopigwa Novemba 3 kwenye Uwanja wa Kinesi.

Cheka na Mbabe wamekuwa na mkwepano wa muda mrefu ambapo yalishawahi kuandaliwa mapambano kadhaa hapo nyuma lakini hayakuwahi kufanikiwa.


Baada ya tambo za muda mrefu, hatimaye Cheka Promotion wakishirikiana na Forogo Promotion wameamua kukata mzizi wa fitina na kuandaa pambano la kumaliza utata na kumtafuta mfalme wa ngumi Tanzania ambalo litakuwa la kilo 78.

Cheka amesema kuwa yeye ni mfalme kwa miaka 10 sasa na kwamba ufalme huo alipewa na rais mstaafu Jakaya Kikwete ambapo alifanyiwa sherehe kubwa kwao Morogoro na kwamba anataka kuwaonyesha watu kuwa bado ni mfalme wa ngumi.


“Mimi ndiyo mfalme wa ngumi Tanzania kwa zaidi ya miaka 10, hivyo lazima nionyeshe watu kuwa mimi ni mfalme kweli, Dulla ajipange na kwenye ngumi hakuna uchawi ni kufanya mazoezi tu kama anahisi atanipiga wakati akiwa hafanyi mazoezi basi nitamtwanga kama mwanangu,” alisema Cheka.


Naye Mbabe ametamba kumtwanga Cheka mapema na kwamba safari hii hana pa kutokea na lazima amuonyeshe na kumtwanga kama mtoto mdogo.

Naye Mkurugenzi wa Golden Promotion, Shomari Kipambau amesema mkanda unaogombaniwa ni mpya na haujawahi kutumiwa mahali popote na utatumika kwa mara ya kwanza.

Mabondia hao walisaini mkataba jana mbele ya mashabiki wa ngumi katika kiwanja cha mpira cha Las Vegas, Mabibo.

Mbali na pambano hilo kutakuwa na michezo mingine ya utangulizi ya raundi 10, 8, 6 likiwemo la wanawake kati ya Rehema Abdallah na Asha Ngedere uzito wa Light Weight kilo 60.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic