October 5, 2018




Beki wa kimataifa wa Simba, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast ameweka wazi kuwa Ligi Kuu Bara imekuwa ngumu kwao lakini kwa upande wake atapigana vya kutosha kuona anaisaidia timu yake ifanye vizuri.


Wawa ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba msimu huu ambapo beki huyo amejihakikishia nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo inayofundishwa na Mbelgiji Patrick Aussems.


Wawa kuwa mipango yake ni kuisaidia timu hiyo ifanye vizuri kwenye mechi zao zinazokuja ikiwa ni baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye mechi yao iliyopita mbele ya Yanga.


“Ligi ni ngumu kiukweli kama inavyoonekana lakini kwetu tumejipanga kuona tunafanya vizuri kwenye michezo yetu.


“Kwangu nataka niisaidie timu iweze kupata matokeo mazuri kwenye michezo ijayo hasa ikiwa ni baada ya kushindwa kufanya hivyo kwenye mechi yetu iliyopita na Yanga,” alisema Wawa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic