MANULA:STARS TUMEPEWA KAZI NGUMU NA TAIFA
Mlinda mlango wa timu ya Taifa Stars, Aishi Manula amesema kuwa wamepewa kazi ngumu na Taifa kuhakikisaha wanapata nafasi ya kuweza kushiriki mashindano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani Cameroon.
Manula amesema furaha ya watanzania ni kuona wanaweza kufanikiwa kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo hicho ndicho kilicho katika akili za wachezaji wote.
"Rais ametuambia maneno magumu ambayo yametupa nguvu ya kuanza kupambana upya hasa kwa michezo ambayo imebaki,kazi kubwa tutaifanya kwa kushirikiana.
"Tuna nia ya kushiriki mashindano ya Afcon na ili tuweze kupata tiketi hiyo ni lazima tuwafunge wapinzani wetu ambao ni Lesotho na Uganda"alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment