MASKINI MTIBWA WAENDELEA KUZILILIA MILIONI HAMSINI ZAO ZA UBINGWA WA FA, HAWAJAPEWA
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar umeendelea kuzililia fedha zake za ubingwa wa Kombe la Shirikisho 'Azam Sports Federation CUP' ilizozipata kwa kutwaa taji hilo.
Mpaka sasa bado Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halijakabidhi fedha hizo kwa Mtibwa ambao walibeba ubingwa ka kuifunga Singida United mechi ya fainali kwa mabao 3-2.
Kwa mujibu wa Msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru, amesema wao kama klabu wanasikitishwa kutokupokea fedha hizo hadi leo.
Kifaru ameeleza kushangazwa na TFF huku akinena hawezi kuzungumza mengi kwa sababu anaweza akaonekana kama tatizo kwa shirikisho hilo.
"Hauwezi amini mpaka sasa bado hatujapokea fedha hizo, nakosa mengi ya kuzungumza na inashangaza kwakweli" alisema.
Mtibwa ilifanikiwa kuwa bingwa baada ya kuilaza Singida mabao hayo matatu kwa mawili, mchezo uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Juni 2 2018.
0 COMMENTS:
Post a Comment