October 13, 2018


Siku chache tangu meneja wa mchezaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu kutamka kuwa kuna baadhi ya timu zimeonyesha kumhitaji mshambuliaji huyo, uongozi wa Klabu ya Yanga umeibuka na kusema hakuna kitu cha bure na yeyote anayemhitaji staa huyo aende mezani wakazungumze ikiwemo Simba.

Ajibu ambaye alisajiliwa na Yanga msimu uliopita akitokea Simba, amekuwa na kiwango bora msimu huu kwani mpaka sasa amehusika katika mabao nane na kutoa asisti sita huku akifunga mabao mawili.

Katibu wa Yanga, Omary Kaya alisema kuwa kiwango cha Ajibu kuongezeka ni jambo zuri na wao kama uongozi wanamuomba azidi kuongeza juhudi zaidi lakini hakuna taarifa ambayo ipo mezani kwake inayohusu timu kumtaka Ajibu hivyo kama wanamtaka waende kukaa mezani na siyo kuongea maneno pembeni kwani hakuna kitu cha bure.

“Taarifa hizo ndiyo kwanza nazisikia kwako wewe ila kwenye meza yangu hakuna barua ya timu ambayo inasema kuwa inamhitaji Ajibu lakini pia hakuna kitu cha burebure duniani, kwani hata ukimtaka mwanamke lazima umtongoze, hivyo kama wanamtaka Ajibu waje mezani tukae tuongee na siyo kuongea pembeni tu, wakija na pesa za kutosha sisi tunamuachia.

“Huwezi ukaanza ligi bila kujipanga, hivyo sisi kama uongozi wa Yanga tumejipanga kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri katika mechi zetu za ligi kuu na kurudisha heshima yetu,” alisema Kaya.

Alipotafutwa Ajibu kuzungumzia ishu ya kutakiwa na timu kadhaa za Uarabuni, Afrika Kusini pamoja na Simba, simu yake iliita bila kupokelewa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic