Kocha Mkuu wa timu ya Simba raia wa Ubelgiji Patrick Aussems, amefumua kikosi cha Simba na kuamua kuja na mfumo mpya ili aweze kushinda leo dhidi ya Stand United utakaochezwa uwanja wa Taifa.
Mbelgiji amefikia hatua hiyo kutokana na safu ya ushambuliaji kushindwa kuwa makini kutumia nafasi wanazozipata.
"Washambuliaji wangu wote wanakosa umakini wanapokuwa katika lango nimeliona na nimelifanyia kazi,nimewapa mbinu mpya ambazo zitasaidia kupata ushindi mapema.
"Kwa sasa kila mchezaji nimemfundisha kufunga kwa mbinu zote ili kuwarahisishia washambuliaji kazi hasa wanapopata nafasi nao wataweza kufunga,natarajia mabadiliko makubwa ndani ya kikosi"alisema.
Acha miguu ya wachezaji iongee,makocha mmekuwa na visingizio vingi na maneno mengi timu inapokuwa imefanya vibaya,Kila kitu kitaonekana uwanjani na sio maneno tumeshayazoea Sana!
ReplyDeletealichosema ndicho kilicbotokea, tumeona team ilivyobadilika na magori 3 yamepatkana, hope next match Salamba starts!
ReplyDelete