October 3, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umesema ratiba ya mechi za Ligi Kuu Bara msimu huu haitasimama kisa kuitwa kwa wachezaji wa Simba na Yanga katika timu ya taifa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, ameeleza kuwa taarifa zilizoandikwa kwenye mitandao mbalimbali kuhusiana na kusimamishwa kwa baadhi ya mechi hazikuwa na ukweli.

Taarifa hizo zilieleza kuwa TFF itasimamisha mechi za Simba na Yanga kutokana na wachezaji wake kuitwa Stars jambo ambalo Ndimbo amelikanusha na kusema ni la kupuuzwa.

Ndimbo amesisitiza kuwa mechi hizo zitaendelea kama kawaida na wachezaji walioitwa Stars si sababu ya kusimamisha ratiba ya ligi kama ambavyo imeripotiwa.

Ofisa huyo amesema kuwa wachezaji walioitwa Stars wataruhusiwa kwenda kuzitumia klabu zao na baada ya kuzichezea watarejea tena kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic