October 6, 2018


Wakati kikosi cha Simba kikitarajiwa kushuka dimbani taifa leo kucheza dhidi ya African lyon, timu hiyo itaendelea kukosa huduma ya mchezaji wake, John Bocco.

Bocco ambaye ni nahodha, ataukosa mchezo huo baada ya kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika mchezo dhidi ya Mwadui FC uliopigwa Septemba 22 2018 huko Shinyanga.

Bocco alipewa kadi hiyo baada ya kucheza mchezo usio wa kiungwana kwa kumpiga ngumi mchezaji wa Mwadui na kupewa kadi ya moja kwa moja.

Nahodha huyo pia alikukosa mchezo uliopita dhidi ya watani zake wa jadi Yanga ambao ulimalizika kwa suluhu tasa ya 0-0.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic