October 6, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umeitahadharisha Mbao FC kuwa hawajaja Dar es Salaam kucheza na SImba.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika, akiwataka Mbao kujipanga vilivyo kwani wamedhamiria kutoa maangamizi.

Nyika ameeleza kuwa Mbao wanajiamini wakijua kuwa wamekuja kucheza na Simba kitu ambacho haitakuwa rahisi kwao kupata matokeo.

Mwenyekiti huyo ambaye pia yupo kwenye kitengo cha Kamati ya Mashindano amefunguka hayo baada ya Mbao hivi karibuni kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao wa jadi Simba huko CCM Kirumba, Mwanza.

"Awamu hii wanaenda kucheza na Yanga na siyo Simba, hivyo wanapaswa kujipanga kwa maana tumedhamiria kuchukua alama tatu" alisema Nyika.

Yanga itakuwa inawaalika Mbao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho Jumapili, mechi ikianza majira ya saa moja za usiku.


4 COMMENTS:

  1. Mwandishi George unakumbuka kabla ya mechi ya Simba na Yanga uliandika eti Nyika amesema kuwa Simba itafungwa 4-0!Ikawa Yanga ndio waliofundishwa soka.labda una tatizo la kukumbuka.Kati ya Simba na Yanga...Mbao ameishakuwa mmbabe wa Yanga Mara nyingi zaidi!Acha kuandika kishabiki!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwenye kumbukumbu inaonyesha Mbao kamfunga Yanga mara 3(2 ligi na 1 azam conf) zote Mwanza na Yanga kaifunga Mbao mara 2(ligi ) zote Dar es salaam.Kwa maana hiyo kila timu inatumia vyema uwanja wa nyumbani hivyo yajayo yanafurahisha!

      Delete
  2. Na uwe unafikiria...sio kila analoropoka Nyika ndio unaona ni habari ya kutuandikia...kwa mweledi wa kazi yako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic