Kocha mkuu wa timu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema Ibrahim Ajibu anauwezo wa kutumikia timu ya taifa endapo ataongeza juhudi na kufikia malengo ya kocha wa timu ya taifa.
Zahera alikuwa kwenye benchi akiongoza timu kushinda mabao 3-0 dhidi ya Aliance amesema kuwa kufunga mabao pekee bado havitoshi kwa Ajibu kuchezea timu ya Taifa .
"Huwa namwambia Ajibu anapaswa aongeze juhudi zaidi,kufunga mabao inategemea na namna ambavyo mpira utamkukuta,kuitumikia timu ya Taifa kunahitaji kujitoa.
"Bado ananafsi ya kufanya vizuri endapo ataendeleza juhudi ,ana kazi kuhakikisha anaweza kudumu katika kiwango chake asiruhusu kidumae , kila siku anabadilika na anaweza kucheza timu ya taifa akiitwa"alisema Zahera.
Brother sasahivi naona umekaa biashara zaidi tangu ujiunge na hilo gazeti lako. Kichwa cha habari hakisadifu kilichomo ndani.
ReplyDeleteKuwa makini sana kutanguliza maslahi mbele maana siku hizi unapoteza mvuto wa habari zako