MOURINHO ABAKI NA SAA 24 UNITED
Muda wa Kocha Jose Mourinho kuendelea kuwepo ndani ya Manchester United umebaki mfupi na hiyo inatokana na Mreno huyo kuendelea kutibuana na wachezaji wake na sasa mbaya zaidi ni kuwa hata mabosi wake wanaelekea kufikia ukomo wa uvumilivu.
Taarifa kutoka klabuni hapo zinaeleza kuwa ikiwa Man United itapoteza mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Newcastle katika Premier League basi kibarua chake kitakuwa kimeota nyasi.
Habari hizo zimepewa n g u v u z a i d i h a s a k w a k u w a k o c h a wa zam a n i w a R e a l M a d r i d , Zinedine Zidane n a y e inaelezwa kuwa yupo tayari kubeba mikoba baada ya Mreno huyo kufukuzwa.
Bodi ya United ilikuwa tayari kumuunga mkono kwa kuwa ndani ya misimu miwili aliyodumu kulikuwa na maendeleo uwanjani tofauti na wenzake wawili waliomtangulia lakini kwa mwelekeo wa timu ulivyo sasa hali inaweza kuwa tofauti.
Siku tatu zilizopita nguli wa United, Paul Scholes alisema anashangaa kuona kocha huyo hajafukuzwa mara baada ya timu kufungwa mabao 3-1 dhidi ya West Ham.
United imeanza msimu vibaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1989, ikiwa imeshatolewa katika Carabao Cup, inazidiwa pointi tisa na vinara wa Premier na ilishindwa kuifunga Valencia, Jumanne iliyopita katika Ligi ya Mabingwa.
Roy Keane amtetea Mourinho
Nahodha wa zamani wa United, Roy Keane amemuunga mkono Mourinho na kusema kuwa kuna ‘watoto wengi wanalialia’ katika soka la sasa.
“Siyo kila mchezaji atapatana na kocha, lakini unachotakiwa kukifanya ukiwa mchezaji ni kutimiza wajibu wako, niliwahi kukwaruzana na makocha kadhaa lakini bado nilicheza kwa faida ya timu.
“Sijali umekwaruzana vipi na kocha au mtu mwingine, unapokuwa Man United utambue ni moja ya klabu kubwa duniani na kuna vitu vitakuzwa, unapovaa jezi ya United unatakiwa kupambana kwa asilimia 100.
“Mchezaji anayegombana na kocha kisha anacheza chini ya kiwango siyo mchezaji, siku hizi kuna watoto wengi wanalialia, namtakia kila la kheri Mourinho kudili na kazi yake,” alisema Keane.
0 COMMENTS:
Post a Comment