October 5, 2018


Staa wa PSG, Neymar, juzi alionyesha kuwa bado anaweza kuonyesha ki­wango cha hali ya juu baada ya kuifungia timu yake mabao matatu ‘hat trick’ walipoichapa Red Star Belgrade mabao 6-1 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mchezo huu umemfanya Mbrazili huyo kuweka rekodi mbili muhimu kwenye maisha yake ya soka.

Moja; alikuwa mchezaji wa kwan­za kufunga mabao mawili ya faulo kwenye mchezo mmoja wa Uefa, kuanzia Cristiano Ronaldo alipo­fanya hivyo mwaka 2009.

Pia alifikia rekodi ya kuwa mche­zaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa wale wazaliwa wa Brazil baada ya kufikisha mabao 30 na kulingana na Ricardo Kaka.

Matokeo haya yanamaanisha mshambuliaji huyo sasa amehusika kwenye mabao 49 katika michezo 49 ya Uefa aliyocheza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic