VIDEO - LAANA YA NAMBA 7 YAMTESA SANCHEZ UNITED
Maisha ya Alexis Sanchez akiwa katika jezi namba 7 ndani ya Manchester United ni magumu na ni kama mwendelezo wa ‘laana’ ya ugumu wa kuitumia jezi hiyo tangu ilipoachwa na Crtistiano Ronaldo mwaka 2009.
Sanchez ameshindwa kung’ara na hivyo kuungana na mastaa wengine ambao waliivaa jezi hiyo klabuni hapo lakini wameshindwa kufanya kweli hasa kwa kuwa jezi hiyo inaheshimika kwa kiwango cha juu klabuni hapo.
Ronaldo alifunga mabao 68 ndani ya Premier League katika miaka sita akiwa United, lakini tangu aondoke wengine wote kwa jumla yao wamefunga mabao 13 katika mechi 138 za Premier tangu kuondoka kwa Ronaldo.
Wakali wengine waliowahi kuitendea haki jezi hiyo klabuni hapo ni George Best, Eric Cantona na David Beckham.
Takwimu za waliovaa jezi no 7 baada ya Ronaldo (katika Premier League)
0 COMMENTS:
Post a Comment