POPPE AKIRI KUSHIRIKI MCHAKATO WA NYASI,KESI KUUNGURUMA TENA
Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba Zakaria Hans Poppe amekiri mahakamani kuhusika katika mchakato wa kununua nyasi bandia kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo.
Poppe amekiri uhusika huo wakati wa kusomewa maelezo ya awali (PH) wa kesi inayomkabili katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu inayomkabili yeye pamoja na Rais wa Simba Evas Aveva na Makamu Geofrey Nyange "Kaburu".
Mashtaka mawili ambayo anakabiliwa nayo Poppe ni pamoja na kugushi nyaraka na kuwasilisha nyaraka za uongo yeye pamoja na wenzake.
Akiwasomea maelezo ya awali (PH) wakili wa Serikali Mwandamizi Shedrack Kimaro akisaidiana na Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa Machi 12,2016 klabu ya Simba ililipwa jumla ya Dola za kimarekani 319,212 na klabu ya Etoile Sportive Du Sahel ya nchini Tunisia ikiwa ni ada ya uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi.
Kesi hiyo itaunguruma tena October 31 ambapo upande wa mashtaka unaanza kutoa ushahidi,
0 COMMENTS:
Post a Comment