Kikosi cha timu ya Azam kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Azam Hans Pluijm amesema kuwa hakuna mwalimu ambaye anapenda kupoteza mchezo,anashangazwa na uwezo wa wachezaji wake hasa wakiwa uwanjani.
" Wachezaji wangu wananishangaza sana kwa juhudi zao wanafuata maelekezo ,wanajiamini wakiwa ndani ya uwanja, bado kazi ni ngumu kwa kuwa kupata ushindi sio kazi rahisi nimewaambia wasibweteke na ushindi walioupata" alisema.
Michezo mingine iliyochezwa leo ni pamoja na ule uliowakutanisha Ndanda na Mbeya City,Mwadui na Ruvu Shooting huku matokeo yao ikiwa ni sare ya bila kufungana.
0 COMMENTS:
Post a Comment