Kocha wa Simba, Patrick Aussems amekiri kwamba kila akiangalia sura za wachezaji wake mazoezi haziko sawa kutokana na tukio la kutekwa kwa mwekezaji mkuu wa klabu, Mohammed Dewji ‘MO’.
Aussems amesema kuwa tangu kutokea kwa tukio hilo, baadhi ya wachezaji wake akili zao hazijakaa sawa na wamejawa na hofu kubwa juu ya kiongozi huyo. Jana jioni Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ilisisitiza kwamba kila kitu kwenye uchunguzi kinafanywa kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha kiongozi huyo anapatikana.
“Tumeanza mazoezi lakini wachezaji walio wengi bado akili zao hazijakaa sawa. Bado wanahofu kubwa juu ya kiongozi huyo kwa sababu hawajui nini hatima yake huko alipo ila najitahidi kuwajenga kisaikolojia ili waweze kukaa sawa na kuendelea na majukumu yako kama kawaida,” alisema Aussems ambaye pia analipwa na MO aliyemleta nchini.
Beki huyo mwenye kilo nyingi na mwili mkubwa ndani ya Simba, Pascal Wawa amesema; “Hatujisikii vizuri kwa jambo hilo maana ni mtu muhimu katika timu yetu lakini jambo pekee kwangu mimi ni kumuombea kwa Mungu.”
James Kotei alisema; “Hadi muda huu bado siziamini hizi habari za kutekwa kwa bosi wetu nahisi kama nipo ndotoni tangu litokee tukio hilo, ila hata mwili umekuwa ukinisisimka sana ninapomuwaza maana hili ni tukio la ajabu sana kulisikia likitokea kwa bilionea mkubwa kama yeye.
“Nilishukuru sana hata uamuzi wa timu kusitisha mazoezi baada ya taarifa hizo kwani wangesema tufanye tu hiyo juzi siku ya tukio hakika ningeshindwa kabisa kufanya kwani tukio hilo limenigusa utasema nimepigwa shoti ya umeme,” alisema Kotei.
CHANZO: SPOTI XTRA
Inshallah
ReplyDeletewachezaji wanafikiria hatma ya mishahara kulipwa
ReplyDelete