October 24, 2018


Kikosi cha Simba kimevuruga mipango ya Alliance FC muda mfupi kabla ya kuanza mchezo uwanja wa taifa leo baada ya kufanya mabadiliko ya kiufundi kwa kumtoa mlinda mlango changuo la kwanza la mwalimu.

Kwa mujibu wa Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema kuwa Kocha wa Alliance ameamua kubadilisha  kikosi chake kwa kumtoa mlinda mlango Said Lubawa ambaye ilibidi aanze.

"Mwalimu ameamua kumtoa Said Lubawa ambaye ni mlinda mlango  nafasi yake imechukuliwa na Kelvin Rashid na benchi atakaa Ibrahim Isihaka kutokana na sababu za kiufundi," alisema.

Alliance ipo chini ya koha Mbwana Makata iliweka kambi yake mkoani Pwani baada ya kupoteza mchezo wake uliopita dhidi ya Yanga kwa kufungwa mabao 3-0.

1 COMMENTS:

  1. kapata alichokuwa anakihitaji,kipa mfupi hana uwezo unampanga mechi ya Simba!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic