October 8, 2018


Ikiwa ni siku mbili tu zimepita tangu Simba icheze na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, kuna hatihati ya kiungo mnyumbulifu wa timu hiyo, Jonas Mkude kuukosa mchezo wa Taifa Stars na Cape Verde.

Taarifa ambazo mtandao huu umezinasa zinasema Mkude aliumia kwenye mechi hiyo ambayo Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Kuumia kwa mkude kunaweza leta pengo kwa Stars na hata Simba haswa kwenye nafasi ya kiungo kwa mechi zijazo kwani haijajulikana lini atarejea kuwa fiti.

Hata hivyo taarifa kutoka kwa Daktari wake, zinasema kiungo huyo anaweza akakaa muda si mrefu nje ya uwanja kutokana na kuumia kwake.

Mkude anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Stars kitakachoshuka dimbani Oktoba 12 kukipiga na Cape Verde kwa ajili ya kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019.


4 COMMENTS:


  1. Obsession na Simba ni hatari kwa afya yako.Mkude hajaumia kiasi cha kuwa headline news.Alikuwa anatembea pekee yake bila msaada.Naona hata mchezaji wa Simba akipiga chafya kwako ni news. Chill out
    kuna timu nyingi za kuripoti.

    ReplyDelete
  2. Ratiba ya ligi kuendelea muhimu lakini wakati huu wa timu ya Taifa ikijiandaa na mchezo muhimu kabisa katika hatima ya la kama Tanzania inaweza kurudi tena kwenye mashindano makubwa Africa basi tutarajie matukio kama haya ya Mkude lazima kutokea kwenye ligi. Mchezaji kama kapombe kutokana na staili yake ya uchezaji kwa wachezaji wetu hawa bongo na marefa wanaoshindwa kuendana na kasi ya mchezo watamuumiza tu. Na ni pigo kwa taifa stars kumkosa mchezaji kama kapombe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic