October 14, 2018


Jumanne jioni nyasi za Uwanja wa Taifa zitatambua kwanini kauli mbiu ya Mbwana Samatta au Genk au Taifa Stars ni haina kufeli. Straika huyo wa akivaa kitambaa cha unahodha ataiongoza Stars kurudiana na Cape Verde kama mechi ngumu na muhimu ya kufuzu Afcon itakayopigwa saa 11 jioni.

Kila kundi zinafuzu timu mbili kwenye fainali za Afcon zitakazopigwa nchini Cameroon. Stars inahitaji kwa udi na uvumba kushinda mechi hiyo baada ya kupoteza mchezo wa ugenini juzi usiku kwa mabao 3-0 huku mashabiki wakilaumu zaidi safu ya ulinzi na kiungo iliyopangwa na Kocha Emmanuel Amunike. 

Kabla ya mechi ya juzi,rekodi zinaonyesha timu hizo zimekutana mara mbili mwaka 2008 kuwania kufuzu Kombe la Dunia na kila mmoja alishinda kwake.

Stars yenye pointi mbili kwenye kundi L, ikishinda angalau mechi zote tatu itakuwa imejihakikishia kufuzu ingawa kundi lake bado liko wazi yoyote anaweza kusonga mbele akizicheza vyema karata zake. 

Stars chini ya Amunike itakuwa na mastaa wake wote wanaocheza nje, kama Thomas Ulimwengu, Farid Mussa, Simon Msuva, Shabaan Chilunda, Abdi Banda na Samatta ambaye ndiye straika namba moja wa Tanzania

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic