October 12, 2018


Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimekubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Cape Verde.

Stars imeweza kuruhusu mabao hayo katika mchezo wa kundi L na kuifanya ibakie na alama zake 2 ikishuka mpaka nafasi ya 4 ya msimamo.

Wakati huo Cape Verde wamepanda juu kwa kufikisha alama 4 kwenye msimamo huo wa kundi L

Timu hizo zitarudiana tena Oktoba 16 2018 kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

6 COMMENTS:

  1. Bora mngeichukuwa simba tu ikacheze kuliko hiyo taifa star yenu mnatumia garama kubwa upuuzi mtupu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba hii hii iliyobanwa mbavu na Ndanda na kufungwa na Mbao!!!!

      Delete
  2. Hii timu bora wamwazime Papaa Mwinyi Zahera ambaye hajafungwa kwenye ligi

    ReplyDelete
  3. Hovyoo.Ni mapema kushusha lawama kutokana na hali inavyokwenda ndani ya timu ya Taifa lakini ukweli lazima tutasema.Ingawa kwa hulka ya mtanzania awe kiongozi wa taasisi fulani au mtu wa kawaida ukimuambia ukweli inakuwa nongwa.Na mara nyingi baada ya kusikiliza ukweli anaoambiwa kwa faida na kujirekebisha huwa anazidisha ujinga ili kumkomoa anaemwambia ukweli huku yeye mwenyewe akiendelea kuharibikiwa,huyo ndio mtanzania. Taifa Stars imeanza kupoteza muelekeo na mvuto pale walipoingia mgogoro usio wa lazima na wachezaji wa Simba kwa kisingizio cha nidhamu. Labda hata uteuzi wa kocha kiuhalisia TFF itakuwa imechemsha ingawa wadau wengi wa michezo nchini wakionekana kufuata mkumbo bila ya kutathmini kwa undani uwezo wa kocha huyo kijana asiekuwa na uzoefu. TFF Walipaswa kuajiri kocha sio jina la kocha na katika listi ya makocha ambao wangetupa matokeo chanya katika kipindi hiki kifupi cha mpito ni makocha amabao wanawafahamu wachezaji wetu wao wenyewe binafsi bila ya kushikwa sikio na mtu mwengine. Kocha kama Mzambia Lwandamina aliekuwa kocha wa Yanga asingetuangusha pengine hata gharama zake zingekuwa po. Kocha mwengine angetufaa kututoa gundu la kufuzu Afcon ni mfaransa wa Simba Lerchante ni kocha ambae anauzowefu tosha na anaufahamu wakati gani wa kuremba na wakati gani wa matokeo. Hivi karibuni kocha wa Simba Mbeligiji alilalamika na kushangazwa kuona wachezaji wanafanyishwa mazoezi magumu wakati zimebakia siku chache kabla ya mechi basi akakomeshwa kwa maneno makali na baadhi ya viongozi wa TFF amabao sidhani kama wanataaluma hata ya ukocha. Katika mechi hii kama mtu alifuatilia utaona baada ya Gadiel Michael kuchemsha nafasi yake ikachukuliwa na Shomari kapombe? Sio Mohamedi Husein shabalala au Haji mwinyi au beki tatu yeyote asilia? Kweli kapombe ni kiraka lakini kiraka huwekwa baada yakuwa hakuna jinsi.kweli kocha ndie mchaguaji na mpangaji wa timu lakini sio siku zote wachezaji wote wanaocheza nje ya nchi lazima wapangwe kwakuwa wanacheza nje. Mwanzo nilidhani kapombe ni majeruhi kuwa ndio chanzo cha kuanzia benchi. Bila ya kupepesa kapombe kama yupo fiti vipi utamuanzisha Khasan kessy? Kama kigezo kucheza nje ya nchi kapombe keshacheza mpaka ulaya. Na licha ya umahiri wa Gadiel Michael ni kijana hodari na bidii lakini kama Shabalala yupo fiti vipi unamuacha nje ya timu ya Taifa? Mohamedi Husein ni mzoefu tayari na mechi za kimataifa kiasi fulani tayari keshapevuka ule ukaptei usaidizi wa Simba hakupewa kwa kubahatisha hapa kitakachokuja kutokea mwisho wa habari ni kuja kujilaumu aaaah huu ulikuwa mwaka wetu huu wa kufuzu Afcon. kama kawaida yetu watanzania ni mahiri wa kusubiri kuomboleza majanga wakati nafasi na uwezo wa kuepusha majanga hayo yasitokee tunao kama wahusika wataacha uzembe.

    ReplyDelete
  4. Kocha huyu ni mwanafunzi wa soka la Africa na hawajui kabisa wachezaji wetu. Kama angekuwa anawafahamu wachezaji asingemuacha Ajibu na Nyoni na asingemuweka benchi Kapombe na kumuingiza Kessy. Yondani angecheza na Banda kushoto angecheza mzoefu Nyoni na kulia alipaswa kucheza kapombe. Nafasi ya ULIMWENGU angecheza Ajibu au Chilunda.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ungekuwa kocha ww ......achen hz watanzania hamjui kt halafu mnajifanya mnajuaaa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic