TFF KUZISHUSHA DARAJA SIMBA NA YANGA, SABABU HII HAPA
Kama utani vile lakini ndiyo hivyo. Unaambiwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupita kwa Mwenyekiti anayehusika na masuala ya leseni za vilabu, Lyod Nchunga, amesema klabu zote ambazo hazina viwanja vyake vitashushwa daraja.
Nchunga ameibuka na kueleza hayo akisema klabu hizo zitashushwa daraja kwa kuwa zinakuwa hazijakidhi kiwango cha kuwa na leseni hiyo.
Mwenyekiti huyo amesema ifikie wakati klabu zote ziwe na viwanja vyao ambavyo vitakuwa vinatumika kwa ajili ya mechi zao za mashindano mbambali ikiwemo Ligi Kuu Bara.
Endapo rungu hilo litapitwa, klabu za Simba, Yanga, African Lyon ni baadhi ya vitakavyoshushwa daraja kutokana na kutokuwa na viwanja vyao.
Timu hizo tajwa hapo zimekuwa zikitumia Uwanja wa Taifa na Uhuru kwa mechi za nyumbani katika ligi na mashindano mengine.
Nadhani kila mtu anataka kusikikana kwenye vyombo vya habari. Ishushwe Simba na Yanga daraja huo mshahara wake utatoka wapi?
ReplyDeleteNikupenda kusikika tu
Delete:))
ReplyDeleteHizo kiki
ReplyDelete