October 5, 2018


Wakati kikosi cha Simba kikiwa katika maandalizi moto ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon kesho Jumamosi, mashabiki wa timu hiyo wameanza kutamba baada ya ujenzi wao Uwanja wa klabu hiyo kuanza juzi.

Simba imeanza kujenga rasm uwanja wake uliopo Bunju pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam ambao itakuwa inautumia kwa ajili ya kufanyia mazoezi.

Mashabiki hao baadhi wameibuka na kusema kwa sasa wamezidi kupata cha kuwatambia watani zao wa jadi Yanga ambao mpaka sasa hawajakamilisha ujenzi wa kiwanja chao cha Kaunda kilichopo mitaa ya Twiga, Jangwani.

Jeuri hiyo wameipata baada ya Mwekezaji wa klabu hiyo, Bilionea kijana Mohammed Dewji 'Mo' kueleza kuwa ameamua kutimiza ndoto yake ya kuijengea Simba Uwanja baada ya miaka 82 kupita.

Mo ameahidi kukamilika kwa ujezi wa Uwanja huo ili Simba iwe inautumia kujifua kimazoezi kabla ya mwezi wa pili mwakani, na sasa itakuwa haitumii tena gharama za kulipia uwanja wa Boko Vetrani ambao mara nyingi imekuwa ikiutumia kufanyia mazoezi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic