October 26, 2018


Bao kali la kiufundi lililofungwa na kiungo mchezeshaji Claytous Chama lilishindwa kumzuia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe na kujikuta akinyanyuka kwenye kiti na kuanza kulishangilia.

Mzambia huyo anayetumia miguu yote alifunga bao hilo dakika ya 87 kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Alliance, alianza kwa 'kusepa na kijiji' cha mabeki baada ya kumchambua Kelvin Richard na  kuwafanya washinde kwa mabao 5-1.

Baada ya kufunga bao hilo, Poppe alishindwa kuvumilia hisia zake na kujikuta akinyanyuka akiwa pamoja na Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallaha "Try Again wakiungana na viongozi waliokaa VIP.

Chama amefikisha jumla ya mabao mawili katika Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kusajiliwa kwa dau la shilingi milioni 60 akitokea timu ya Power Dynamo ya Zambia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic