October 5, 2018





Unaweza kusema mambo siyo mazuri kwa straika wa Yanga na mfungaji bora mara mbili katika Ligi Kuu Bara, Amissi Tambwe baada ya kutupwa pembeni katika timu ya taifa ya Burundi ambayo inajiandaa kucheza dhidi ya Mali kwenye michezo ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Kombe la Afrika (Afcon) mwakani.


Tambwe amekuwa na wakati mgumu tangu msimu uliopita ambapo alipata majeraha ya goti ambayo yalimuweka nje kwa muda mrefu.


Mshambuliaji huyo alirejea uwanjani hivi karibuni na kuisaidia Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida United ambapo alifunga mabao yote mawili.


Wakati mshambuliaji huyo wa Yanga akitupwa nje ya kikosi hicho cha Burundi kitakachocheza na Mali, Oktoba 12, mwaka huu straika anayecheza soka la kulipwa katika Klabu ya Stoke City ya England, Saido Berahino ameitwa kwa mara ya kwanza ndani ya timu hiyo baada ya kuomba kuichezea timu hiyo kutoka ile ya England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic