October 20, 2018

KLABU ya Simba inatarajia kuanza kampeni za uchaguzi rasmi wiki ijayo mara baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa vyeti vya wagombea ambapo baadhi yao vimeonekana kuwa na matatizo.


Simba inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu Novemba 4, mwaka huu kuchagua viongozi wapya baada ya wale wa awali kumaliza muda wao wa kuongoza ambapo awali walikuwa wakisubiria barua kutoka katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kutoa maamuzi juu ya wagombea ambapo imeonekana baadhi yao vyeti vyao vina upungufu.


Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Boniface Lihamwike ameeleza kuwa, wanasubiria ripoti juu ya baadhi ya wagombea ambao vyeti vyao vimeonekana kuwa na ukakasi kidogo ndipo waanze kampeni wiki ijayo.


“Kuna mambo tunayamalizia yanawahusu mgombea mmojammoja, kuna baadhi ya vyeti vya wagombea vina matatizo kidogo, hivyo tunalishughulikia suala hilo.


“Tunatarajia kuanza kampeni zetu wiki ijayo baada ya mchakato kukamilika ila siwezi kuwaweka wazi wagombea ambao vyeti vyao vimeonekana kuwa na matatizo,” alisema Lihamwike.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic