October 20, 2018


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo Dewji amepatikana ikiwa ni siku 9 baada ya kutekwa na watu wasiojulikana October 11, katika Hotel ya Colessium iliyopo Masaki.

"Mo amesema watekaji hao walitaka fedha. Hata hivyo yeye aliwasisitiza kumpigia baba yake kwa kuwa yeye alikuwa nao pale," alisema.


“Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama"alisema Mo

Mo ameungana na familia yake akiwa salama baada ya kupatikana usiku wa kuamkia leo kutokana na watekaji hao kumuachia wakitumia gari lilelile walilotumia kumteka.



2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic