October 8, 2018


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa wachezaji wa kimataifa wameanza kuwasili nchini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2019.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho hilo, Clifford Ndimbo ameeleza kuwa baadhi ya wachezaji wameshawasili akiwemo Thomas Ulimwengu.

Mbali na Ulimwengu, Ndimbo amesema wengine wanatarajiwa kuwasili ikiwemo Mshambuliaji Rashid Mandawa anayekipiga BDF XI ya Botswana akitarajiwa kuwasili kuanzia leo.

Wachezaji hao wataungana na wenzao ambao wapo kambini kwa ajili ya kuendelea na maandalizi kuelekea mechi na Cape Verde.

Taifa Stars itashuka dimbani Oktoba 12 kucheza na Cape Verde nchini kwao ukiwa ni mchezo wa kundi L,

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic