YANGA YAONDOKA NA USHINDI TAIFA KWA KUICHARAZA MBAO 2-0
Dakika 90 zimemalizika kutoka Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa mchezo wa ligi baina ya Yanga na Mbao FC kumalizika kwa wenyeji kushinda mabao 2-0.
Bao la kwanza limepachikwa kimiani na Rafel Daud mnamo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza kwa njia ya kichwa kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajibu.
Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika, kipindi cha pili Mbao walijitahada kuja kwa kasi kushambulia lango la Yanga lakini haikuweza kusaidia kitu.
Licha ya mashambulizi hayo, Mbao FC walipata nafasi zingine kama nne kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuzitumia vema.
Zikiwa zimeongezwa dakika tano, Ibrahim Ajibu alifanikiwa kuingia kambani kwa kufunga bonge la bao kwa tikitaka ya aina yake na kuifanya Yanga iwe mbele kwa mabao 2-0.
Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 2 na Mbao FC 0.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 16 katika msimamo wa ligi huku Mbao ikisalia na alama zake 14 kwenye nafasi ya 5.
Yanga mbele daima,nyuma mwiko
ReplyDeleteHongereni kutumia vyema uwanja wa nyumbani
ReplyDelete