October 6, 2018


Wachezaji wanne wa kikosi cha Simba waliokuwa wameitwa kwenye kambi ya Taifa Stars, wamerejeshwa katika klabu yao kwa ajili ya mechi ya leo dhidi ya African Lyon.

Simba watakuwa wanacheza na Lyon kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo kipute kitaanza majiya ya saa 1 kamili za usiku.

Aishi Manula, Shomari Kapombe, John Bocco na Jonas Mkude ndiyo wachezaji wa Simba waliokuwa wameitwa kambini Stars kwa ajili ya kujifua kujiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde.

Cape Verde watakuwa wanaialika Stars nchini kwao, ambapo mechi hiyo ya kundi L itapigwa Oktoba 12 2018.

Aidha, wachezaji wengine waliorejea kwenye klabu zao ni wale wa Mtibwa Sugar ambao wataitumikia timu yao inayoshuka dimbani kucheza na KMC ya Kinondoni huko Manungu, Morogoro.


5 COMMENTS:

  1. Kwa simba hii hata wakiwakosa wachezaji saba na kutokana na hazina kubwa ya wachezaji waliokuwa nayo, haitotetereka hata kidogo

    ReplyDelete
  2. Acha kujidanganya mbona waliandika barua kuomba mechi yao na Biashara isogezwe mbele ili wajiandae kwa mechi na Yanga.

    ReplyDelete
  3. Acha pumba ww,akikosekana mkude na manula tu mnajamba,japo mmeshwahi kutobolewa mkiwa na haohao mnaowasema kikosi kipana.

    ReplyDelete
  4. Hakuna kikosi kama cha simba Africa kwa sasa. Hata zamalek hapana timu yenye wachezaji wa maana kama simba

    ReplyDelete
  5. Wacha kutudanganya simba ni wazuri kwa Yanga tu labda sana sana na timu za ukanda wa Africa mashariki na kusini hadi South Africa na zambia tu lakini sio kwa Africa nzima. Huko wasahau. Hawana lolote zaidi ya kuendelea kuionea na kuinyanyasa yanga tu kimpira. Kama kweli wanaweza basi wapige mpira uliokwenda shule kwa timu za Africa kama walivyopiga katika mechi yao na yanga ndio tutasema wako vzr kwa Africa. Sio mnyonge wao kwa mpira ulioenda shule uwe kwa yanga tu ambayo kweli bila uchawi hawawezi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic