November 19, 2018




Timu ya Shinda Zaidi na SportPesa imefika mkoani Kigoma, Mwanga Majengo kwa ajili ya kumkabidhi mshindi wa Bajaji droo ya 28 Bwana Amri Nicolas Junya.


 Timu ya SportPesa ilifika mpaka nyumbani kwao ambako ndiko makabidhiano yalifanyika huku tukio hili likishuhudiwa na wazazi wa Amri, majirani sambamba na wawakilishi wa SportPesa 


Nicholaus anasema hajawahi kubahatika kushinda na hii ndio imekuwa mara yake ya kwanza katika maisha yake hivyo yeye na familia yake kwa ujumla wamelipokea jambo hili kwa uzito mkubwa sana 


"Kupitia bajaj hii niliyoipata kwanza kabisa nina uhakika ndani ya mwaka mmoja kununua uwanja na baada ya hapo nikiweka mipango mizuri ntaanza suala la ujenzi kwa kuwa mpaka hivi sana bado nakaa nyumbani mbali ya hilo naweza kuanza biashara ya dagaa yani nakuwa nasafirisha kwenda mikoani naamini hayo yote ntafanya kutokana na kipato ntakachoingiza kupitia bajaji hii" alisema Nicholaus.


Joseph Mussa Fundi ni baba mzazi wa mshindi na yeye aliupokea ushindi wa mwanae kwa furaha na kuamini kuwa taa ya ushindi imeweka katika familia yake.


"Mwanangu aliniambia bajaj iko njiani wala hata sikuamini akanisisitiza tena kuwa leo saa nne mtakuja mkabidhi ilikuwa ngumu kuamini lakini sasa ndio naaamini kweli nimefurahi na hata wadogo zake wakija kuniomba pesa ya kucheza ntawapa ili tushind nyingine, Si unaona umri wangu unaenda sasa najua mwanangu atanitunza vyema kutokana na kipato atakachopata kutoka kwa bajaji tunashukuru sana SportPesa, " alisema Mzee Fundi.

Kumbuka kila mtu ana nafasi ya kucheza na sportpesa muhimu uwe na umri unaoanzia miaka 18 kuendelea unajisajili kupitia simu yako ya mkononi kwa kupiga *150*87# utaweka pesa kwa kubonyeza namba 7 na kuanza kucheza. Wakati huo huo kwa watumiaji wa mitandao mingine namba ya kampuni ni 150888 na kumbukumbu namba ni 888 kwa ajili ya kuweka pesa kwenye akaunti ya SportPesa na kuanza kucheza mara moja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic