November 19, 2018


Uongozi wa timu ya Simba umemkingia kifua Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emannuel Amunike kutokana na kikosi alichopanga katika mchezo wa jana dhidi ya Lesotho kushindwa kupata matokeo.

Stars jana walikuwa na nafasi ya Kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kama wangeshinda dhidi ya Lesotho ila walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 hali iliyofanya kuongeza mzigo wa kuweza kufuzu Fainali hizo.


Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema hawezi kuzungumzia kikosi kilichopangwa na mwalimu kwani kuna wachezaji wa timu ya Simba, ila kinachotakiwa ni umakini watanzania wanahitaji ushindi.


"Tulikuwa na nafasi ya kumaliza mchezo mapema, kuhusu upangaji wa kikosi hilo ni suala la Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) inabidi waangalie kwa kuwa nafasi tuliyoipata jana haijawahi kutokea ila Mungu anapanga nasi tunapanga.


"Kwa matokeo ya jana ni sawa na kuvuliwa nguo maeneo ya Posta pale huwezi kuchutama inabidi ukimbie, maana jana nimelala na viatu kama vile nimecheza," alisema.







Matumaini ya timu itakayoungana na Uganda Cameroon kwa kundi L ni mpaka mwakani watakapocheza michezo yao ya mwisho kwani Stars na Lesotho wana pointi 5 wote wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

4 COMMENTS:

  1. hahahahah manara sawa ila kocha out #hatumtaki

    ReplyDelete
  2. Ujinga mtupu, Karia bado anamuwakilisha bosi wake Jamali Malinzi alieiongoza TTF fisadi na iliofeli kuwahi kutokea katika historia ya uongozi wa chama cha mpira nchini. Mfano wale akina Hemedi Moroco wanafanya nini pale Taifa stars na wanamsaada gani. Wadau tukisema ukweli tunaonekana wakorofi. Na kwa uongozi huu na nenchi hili la ufundi kama kweli waganda watakuwa serious katika mechi ya mwisho basi watanzania tusahau taifa stars kufuzu.

    ReplyDelete
  3. Kweli chungu lakini kwa uwezo wa kazi aliuonesha Amunike katika kuiongoza Taifa stars basi watanzania lazima tuwaombe radhi akina Julio na makocha wengine wazawa. Maana nina hakika kama Amunike angempisha Jamuhuri kiwelu ama Julio kuiongoza Taifa stars angalau kwa mechi ya Jana tu basi hii leo watanzania mitaanai kwetu hivi sasa kungekuwa kunanuka harufu ya pilau la furaha. Mimi sio kocha lakini wataalamu wa mpira kote duniani wanakauli isiopingwa inayosema ili kupata matokeo chanya uwanjani basi lazima (The best difference of any team is the better offensive) yaani ubora wa beki wa timu yoyote ile katika kujilinda basi utasindikwa na ubora wa safu yake ya ushambuliaji. Sasa huyu Amunike na watu wanaomuongoza lakini mbona anawalazimisha watanzania kuachana na masuala ya soka? Pole sana muheshimiwa raisi Magufuli ila utambue wakati CCM na nchi inateseka kuna watu ama baadhi ya viongozi walituaminisha kuwa hali hiyo ilikuwa ya kawaida na kulikuww hakuna haja ya watu kupiga kelele mpaka ulipokuja kuleta mageuzi. Watanzania wengi ni watu wenye uchungu na kuipenda nchi yao ila kwa kiasi kikubwa wanaangushwa na suala la baadhi ya viongozi wabovu. Tatizo la Taifa stars ni tataizo la uongozi mbovu wa taasisi inayoisamamia timu hiyo. Tuwe wa kweli kabisa watanzania huwa tuna mawazo ya kijasiri na kufikiria kufanya makubwa katika mambo ya hovyo na wakati mwengine kudiriki kutekeleza unyama huo lakini wakati huo huo watanzania tumekuwa waoga na wazembe katika kufikiria mambo makubwa ya manufaa kwa nchi yetu. Wakati Magufuli akiamini kuwa Taifa stars inaweza kwenda Afcon na kuchukua ubingwa wa mashindano hayo wapo wanaombeza kwa maneno lakini mbaya zaidi wapo wanaombeza kwa vitendo, lakini huyo ndio Magufuli na atabaki kuwa Magufuli miongoni mwa watanzania waliowengi na atabaki kuwa Magufuli kwani ni mtu mwenye kuwaza makubwa ya maana na sio kuwaza tu bali anadirki kuyafanya kwa vitendo. Amunike ni jina kubwa katika mpira wa Africa lakini sio kocha mkubwa yaani ni sawa na kumlazimisha rubani mahiri wa ndege mwenye rutini ya kusafiri kutoka Mwanza Dar kuipeleka ndege China ni tendo la kubahatisha ni vyema kutafuta rubani aliekuwa tayari anauzoefu na safari hiyo ya China. Kama Amunike alitaka kujilinda ugenini katika mechi ya Jana na Lethoso basi kikosi chngu cha ushindi kingukuwa hivi(1) Manula(2)Nyoni(3)GADIEL(4)Morris(5)Kevin Yondani(6)Abdi Banda(7)Saimoni msuva(8) Jonas Mkude(9)John Rafael Boko(10) Feisal Salum na kumi na moja(11) kichuya. Abdi Banda ni miongoni mwa viungo mahiri hasa namba sita labda watu hawaelewi hilo na ili kuongeza zege kwenye kisiki cha jiwe basi muweke Banda mbele ya beki kama Yondani na wala sio Mao mkami. Chilunda ni mchezaji anaecheza nje lakini bado yupo kwenye makuzi si wa kuanza wakati wapo wachezaji wazoefu. Lakini bado utaona kama kuna bifu kati ya uongozi unaosimamia Timu ya Taifa na wachezaji wa Simba na Yanga. Kana kwamba wanataka kuonesha wachezaji wanaotoka vilabu hivyo si muhimu na taifa stars itafanya vizuri bila uwepo wa wachezaji wa Simba na Yanga sasa siasa za aina hiyo ni hatari kwa afya ya Timu yetu ya Taifa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakuunga mkono kwa kila ulichokiandika. Ila kwa kuweka wazi, bado Lugha inabaki kuwa Mwenye maamuzi ya mwisho juu ya nani na nani wapangwe kwenye kikosi ni Kocha. Hivyo ni rahisi sana kusema UBAGUZI WA WACHEZAJI ANAULETA KOCHA. Na zaidi naona kama Mkude ndo anaonewa zaidi na AMUNIKE. Nakumbuka hata safari ya kwenda Cape Verde ambako tulipigwa 3 kwa mtungi, Mkude alikuwa ana nafasi ya kwenda ingawa alikuwa ametoka kuwa majeruhi, lakini alikuwa tayari amesha-recover, ila kocha akamuacha na kupata kisingizio kuwa bado hayupo fiti. Sasa hii ya juzi atatuambia nini kuhusu Mkude na wenzake?!!! Mimi nalia na Kocha tu. Tuwe wepesi kwenye maamuzi kwa watu ambao wanaturudisha nyuma kama hawa. Hatua ya kwanza ianzie kwake kocha then uongozi nao wa TFF unaosimamia timu ya Taifa nao uchunguzwe, watakaobainika wachukuliwe hatua. Maana Milioni arobaini zilizotolewa na Rais ni Kodi yetu watanzania.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic