November 8, 2018


Timu ya Lipuli FC ya Iringa iliyo imeendelea kukumbwa na matokeo mabaya baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya Mwadui FC kwa kupoteza mchezo wake wa leo kwa kufungwa bao 1-0.

Huu unakuwa ni mchezo wa tatu kupoteza ugenini, baada ya kuanza kupoteza mbele ya Yanga kwa bao 1-0, African Lyon 2-0 na leo  Mwadui FC 1-0.

Katika mchezo wa leo mchezaji wa Lipuli Seif Karihe alipata kadi nyekundu dakika ya 70 na kufanya wacheze wakiwa pungufu.

Kocha wa Lipuli Seleman Matola amesema kuwa matokeo hayo ni kutokana na wachezaji wake kukosa umakini wa kumalizia nafasi za mwisho wanazotengeneza ila kwa kuwa ligi sio mchezo wa mtoano watajipanga kwa ajili ya michezo mingine.

Matokeo hayo yanawafanya Lipuli kwa nafasi ya 17 wakiwa na pointi 12 baada ya kucheza michezo 13, Mwadui wanafanikiwa kuwa nafasi ya 14 pointi 13 wamecheza michjezo 13.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic