November 21, 2018

Uongozi wa timu ya Azam FC, umejitangazia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao unashikiliwa na Simba FC, kutokana na kuwa nafasi ya kwanza na kucheza michezo 12 bila kupoteza wakiwa na pointi 30.

Ofisa habari wa Azam FC, Jaffari Maganga amesema kuwa hakuna ubishi kwa sasa kikosi bora ni Azam na endapo kutatokea na janga kwenye taifa wataiwakilisha nchi.

"Kwa sasa ipo wazi sisi ndio mabingwa maana kama bahati mbaya kutatokea na majanga ya asili, basi bingwa ni Azam FC, nasi tutawaakilisha nchi kwenye michuano mikubwa tunapaswa tuheshimiwe," alisema.

Kesho Azam FC watacheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa Chamazi majira ya saa moja usiku ikiwa ni mwendelezo wa Ligi kuu.

9 COMMENTS:

  1. Hata raundi ya kwanza haijaisha mnaanza tambo! Kwani mmeshacheza na Mnyama? Kuna mechi nyingi za away pia mtapoteza, Ni mapema mno kuanza tambo.

    ReplyDelete
  2. Hata mzunguko wa kwanza bado umeanza tambo pole sana ila jitahidi kila jambo linawezekana.

    ReplyDelete
  3. Nafikiri msemaji hana jipya kwake ameona mechi 12 ni za kutangazia ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

    ReplyDelete
  4. Omary Kausimbe,
    Hayo ni maneno ya mkosaji huyo msemaji wa azam naona hana cha kuongea teh teh

    ReplyDelete
  5. Unaomba kuheshimiwa kwa kuongoza ligi baada ya michezo 12 unashindwa kutoa heshima kwa bingwa mtetezi mana kombe halitolewi pakitokea majanga kama unavyoomba wewe yatokeee

    ReplyDelete
  6. Cheche hajui kuwa leo Alhamisi pia atakuwa na kazi nzito usiku?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic