Imeelezwa kuwa Uongozi wa Yanga upo kwenye mkakati wa kumuacha mshambuliaji wake wa kimataifa na mfungaji bora kwa misimu miwili, Amiss Tambwe kutokana na kile kilichoelezwa kiwango chake kutomridhisha kocha Mkuu Mwinyi Zahera.
Tambwe amekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu hata baada ya kurejea amekuwa akishindwa kuonyesha ubora wake kwani mpaka sasa ana mabao 2 tu ndani ya ligi kuu.
"Bado hajaweza kumpa nafasi na anatafuta mbadala wake kwa sasa ndio maana hapati nafasi kwenye kikosi kwa sasa huenda akaondolewa ndani ya kikosi cha Yanga, hata Donald Ngoma pia naye majeruhi yalimponza akaruhusiwa kuondoka, sasa anafanya vizuri huko aliko," kilisema Chanzo.
Zahera alisema kuwa kinachomponza Tambwe kushindwa kufanya vizuri ni kutokana na uzito alionao pamoja na kupenda kula ugali hali ambayo inamfanya awe mzito akiwa uwanjani.
Kula ugali 😂 😂 😂
ReplyDelete