Baada ya zoezi la uchaguzi wa Yanga kuelezwa kuendelea na kusimamiwa na kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) tayari wanachama wameanza kuchukua fomu hizo.
Uchaguzi wa Yanga unakuja kutokana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji Kujiuzulu pamoja na wajumbe wengine hali ambayo imepelekea kukaa muda mrefu bila Uongozi.
Kwa upande wa Wajumbe waliochukua fomu ni pamoja na Hamad Ally,Benjanmin Jackson, Silvestoer Haule, Musa Katabaro,Said Baraka, Pindu Luhoyo, Dominic Francis na Jeko Jihadhari.
Kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti ni Dr. Jonas Tiboroha na aliyechukua fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Yono Kevela.
0 COMMENTS:
Post a Comment