November 13, 2018







Klabu ya KMC inayoshiriki Ligi Kuu Bara imemtangaza mshambuliaji Elius Maguri kuwa mshambuliaji wake mpya.

Maguri ameingia mkataba wa mwaka mmoja na KMC kwa ajili ya kuitumikia katika msimu huu wa 2018/19.

Maguri aliyewahi kung'ara na Stand United, Simba alikwenda kucheza soka nchini Oman.

Baadaye aliamua kurejea nchini na kuweka kambi ikielezwa angekwenda nchini Afrika Kusini kabla ya kupotea katika medani ya soka hadi leo alipoibukia KMC.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic