November 19, 2018



Ikiwa zoezi la kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Yanga likiwa bado linendelea, kiongozi wa zamani wa klabu hiyo, Abbas Tarimba, amesema hataweza kuwania nafasi ya Yusuf Manji.

Tarimba ambaye alikuwa naapewa nafasi kubwa ya kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya klabu hiyo, ameeleza kuwa hawezi akachukua fomu hiyo.

Tarimba ambaye ameajiriwa na Kampuni ya SportPesa, ameeleza kuwa kwa sasa ni vigumu kwake kufanya hivyo kutokana na kubanwa na majuku mengine ya kikazi.

Ameeleza kuwa yeye atasalia kuwa mwanachama wa kawaida na pale inapobidi anashiriki katika majukumu ya kuifikisha mbele Yanga ili iweze kufanya vema zaidi.

Tayari wanachama mbalimbali wameshachukua fomu katika nafasi za Uenyekiti na Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambapo uchaguzi utafanyika Januari 13 2019.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic