November 19, 2018


Na George Mganga

Kama utani vile lakini ndiyo hali ilivyo kwa mashabiki wengi wa soka hapa nchini wamelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfukuza kazi mara moja Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike.

Hatua hiyo imekuja na kikosi cha timu hiyo kuambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Lesotho katika harakati za kuwania kufuzu kuelekea AFCON huko Cameroon mwakani.

Mashabiki wengi wameeleza kutoridhishwa na upangwaji wa kikosi cha Stars na Amunike jambo ambalo wanaamini limesababisha kupoteza kizembe.

Wengi wao wamesema kitendo cha kuwaacha nje wachezaji kama Feisal Salum, Jonas Mkude na John Bocco kumesababisha timu ishindwe kuonesha kiwango chake.

Wameeleza timu ilikuwa na mapungufu zaidi haswa sehemu ya kiungo wakiamini kukosekana kwa Mkude imekuwa kama pigo ambapo kikosi kiliwa hakina mhilimili mzuri katika safu hiyo.

Stars sasa inapaswa kuiombea Cape Verde iweze kuifunga Lesotho au kwenda sare mechi ijayo huku nayo ikitakiwa kuwafunga Uganda, The Cranes ili kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCONN) mwakani nchini Cameroon.







11 COMMENTS:

  1. KAMA KIGEZO NI KUFUNDISHA TIMU VIZURI ISHINDE BWANA AMUNIKE MPAKA SASA AMEFELI. AONDOKE TUU. TANZANIA NI TIMU YAKE YA KUIFANYIA MAJARIBIO HATUTAKI. MBONA TFF MNAMVUMILIA SANA AU MNAGAWANA POSHO ZAKE? TIMU ANAIPANGA KAMA HAKUWA MCHEZAJI? LESOTHO? LESOTHO NDIO YA KUIFUNGA TANZANIA? IMETOSHA OUT

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uzuri wetu Watanzania ni ujuaji. Tunajua kila kitu na hatuhitaji kujua tusiyoyajua wala kuheshimu weledi ya kuyakiri mapungufu yetu. Miaka ya 80 tulipata mtaalamu "Mshauri wa soka toka Fifa na pia mtaalamu huyo alipata kufundisha timu maarufu hapa nchini katika miaka hiyo lakini mwisho wa siku alisema "wachezaji wa Tanzania hawafundishiki" kauli hiyo ilifanya aonekane adui na mbaguzi!!! Badala ya kuichukua kauli ile na tukajitathmini ili kuondoa mapungufu yetu na hakika tungesogea mbele. Kwani mtaalamu yule alikwenda kuwa mshauri wa soka China na matokeo yake yanajulikana. Tunapenda kuvuna tusivyovipanda na laiti soka lingechezwa midomoni na magazetini tungelichukua makombe yote pasi shaka. Soka linahitaji nidhamu nasi hatuna nidhamu ya soka tunataka matokeo yetu ya mfukoni!!! Wachezaji hupewa maelekezo na makocha wakiingia uwanjani wanacheza kivyao analaumiwa kocha!!! Midhali miujiza ingaliko nasi UKWELI HUWA HATUUPENDI, TUENDELEE KUTARAJI KUVUNA NANASI KWENYE MKONGE!!! Wachezaji na viongozi wa soka wasipojua soka linahitaji nidhamu na kufuatwa misingi yake si siasa na bhangi ndipo tutavuka. Mashuleni hakuna elimu ya soka na michezo mingine ajabu sana hii sisi kutarajia mafanikio ya waliojiandaa. Tunamfundisha mbwa mzee kuwinda sungura na vicheche wasipomshinda mbio atang'oka meno...

      Delete
    2. acha kukariri.vizazi vinaenda vinabadilika,kama kweli watanzania hawafundishiki!wako wapi akina mbwana sammata,chilunda,moris,msuva nk,kwani huko walipo wanafundishwa na robots?kuna dhana hazipaswi kubebwa na kuutukana utanzania wetu.tff lazima wajue kuna tofauti kati ya kucheza mpira kwa mafanikio makubwa na kufundisha kwa mafanikio makubwa,taaluma ya ukocha aihitaji majaribio,hasa inapogusa timu ya taifa ambayo ni moyo wa wanzania.wastaarabu wote na wenye hekima,husikia na kufanyia kazi maoni chanya,wenye kiburi hujenga hoja ya utetezi juu ya makosa yao.ndivyo alivyo Amunike

      Delete
    3. acha kukariri.vizazi vinaenda vinabadilika,kama kweli watanzania hawafundishiki!wako wapi akina mbwana sammata,chilunda,moris,msuva nk,kwani huko walipo wanafundishwa na robots?kuna dhana hazipaswi kubebwa na kuutukana utanzania wetu.tff lazima wajue kuna tofauti kati ya kucheza mpira kwa mafanikio makubwa na kufundisha kwa mafanikio makubwa,taaluma ya ukocha aihitaji majaribio,hasa inapogusa timu ya taifa ambayo ni moyo wa wanzania.wastaarabu wote na wenye hekima,husikia na kufanyia kazi maoni chanya,wenye kiburi hujenga hoja ya utetezi juu ya makosa yao.ndivyo alivyo Amunike

      Delete
  2. hakuna kocha nayemchukia kama huyu ana kiburi ,jeuri sana iweje banda,mkude,boko wawe benchi kessy benchi huku akijua kapombe na samata hawapop,huyu ni shenzi na mse,,,,,nge ni bora atimuliwe makosa km hayo alifanya cape verde jana tena kayarudia sheeeeeeenz

    ReplyDelete
  3. Kocha aliboa na upangaji wake wa kubahatisha.beki mbili na tatu hazikuwa zinapanda au pengine alikuwa anatafuta sare au goli la kustukiza.kocha alipaswa kujua ilikuwa tulazimishe muda mwingi mpira unachezwa kwenye eneo la kwao walesetho ili kuwachosha ktk kujilinda lkn hatukuwa na viungo wengi na hili kosa limejirudia kama tulivyocheza na Cape Verde huko kwao Praia.Pengine ushauri wangu ni kuwatafuta makocha wa kigeni ambao wameshafundisha clubs zetu za nchini/east Africa kama kina Hans Plujim,Circovic,Brenda,au hata kina Micho a

    ReplyDelete
  4. Nimefuatilia CV ya huyo kocha kumbe hana lolote la kuonyesha. Hajawahi kufundisha timu yoyote ya maana na kuipa mafanikio. Sijui ilikuwaje akapewa ukocha wa Taifa Stars. Aondoke upesi sana!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shida iko ZFF, rais na katibu wake siyo wazawa wa Tanzania wamepigania kuununua uraia ili kupata nafasi kama hi waweze kupiga na wanapiga mno mojawapo kupitia kocha kigezo kipi kimetumika kumleta Ammunike kuwa kocha wa stars kwani hajawahi kufundisha taifa lolote lile na hana sifa lkn pesa anayilipwa ambayo nina hofu kuwepi kwa ten percent ni ndefu kuliko aliyokuwa analipwa kocha fundi poulsen. Takukuru waingilie kati swala hili ili kumwuunga mkono mheshimiwa Rais Mafhufuli ktk kupambama na rushwa, wkt huo huo Amunike aondolewe haraka

      Delete
  5. Jinga kweli anatumia staili ya Zahera.wakati yuko ugenini..Kipindi cha pili Taiga wamecheza na kutawala mpira..Cha kwanza umiliki mpira wa star ilikuwa chini ya asilimia 40..usitegemee shinda kama unazidiwa.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli wakati anaajiliwa TFF walimfagilia utadhani wamepata mchezaji jembe.Hatukuwa tunahitaji mchezaji Bali kocha

    ReplyDelete
  7. Na ndio maana walikuwa hawataki kumtangaza mapema, kumbe tatizo lake watakuwa walikuwa wanalijua kuwa ndio anakuja kufanya field ya ukocha. Na aende tu. Wachezaji ni wazuri ila namna ya kupanga kikosi ndio kachemka. Jana tulitakiwa kucheza JIHADI ili tushinde tufikishe point 8, na ndio lilikuwa lengo, nina imani hata kauli ya Rais wetu ilimaanisha hivyo, na sio kuweka mabeki sita wote, ili iweje! kiungo bado unaweka watu ambao sio nafasi wanazochezea hata kwenye timu zao, unataka uwafundishe upya namna ya kuchezea nafasi kwenye mechi critical kama ile! kwenye mechi kama ile unamuachaje BOKO, unamuachaje FEISAL, unamuachaje KICHUYA, hawa wote unawaachaje eti unamuingiza kichuya dkk ya 79 baada ya kufungwa! unamuingiza boko dkk ya 92 zikiwa zimesalia dkk 8 mpira kuisha! watafanya maajabu gani hawa kwa muda huo ili kurudisha gori na kuongeza la ushindi! maana lengo lilikuwa ni ushindi. RAIS WETU, ulipowakabidhi yale mamilioni, ulisema kuwa wakifungwa watarudisha kwa namna yoyote ile, naomba huyu Kocha ahusike peke yake kurudisha mamilioni yale kabla hajapanda ndege kwenda kwao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic