November 19, 2018


Timu ya taifa ya Tanzania jana imefungwa bao moja bila na timu ya taifa ya Lesotho katika mechi ya kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika nchini Cameroon mwakani

Baada ya matokeo hayo Stars sasa inalazimika kushinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Uganda itakayopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kocha wa timu hiyo Emmanuel Amunike amesema Stars haikua na bahati katika mechi hiyo baada ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga bila kufanikiwa.

7 COMMENTS:

  1. UPUUZI KOCHA WA MAANA UNAZUNGUMZIA BAHATI? HUZUNGUMZII KUTOPANGA WACHEZAJI VIZURI? BOCCO TOP STRIKER NCHINI UNAMUINGIZA DAKIKA ZIMEBAKIA TISA AKAFUNGE GOLI? AMUNIKE UNATUKOSESHA AFCON ATOKE TU

    ReplyDelete
  2. BAHATI? HUYU VIPI? KWANI MIPIRA MINGAPI FOWADI YETU IMEIPIGA GOLINI MWA LESOTHO? WALIOKOSA BAHATI NI LESOTHO MAGOLI ZAIDI YA 3 YA WAZI WAMETUKOSAKOSA. WAO NDIO KWELI HAWAKUWA NA BAHATI. KOCHA AMUNIKE TUACHIE TIMU SASA ONDOKA

    ReplyDelete
  3. Hivi matokeo ya awali kwanini hatukushinda nyumbani? Tunavuna tulichokipanda hata akija Pep Guadiola kwa aina yetu ya misingi ya soka na wachezaji wetu hakuna tutakapoenda. Kweli kabisa tunapenda vitu vizuri lakini hatuhangaiki kujua vinapatikanaje. Ni kama tunaotamani nyumba nzuri tusiyoijenga. Soka ni misingi na misingi hiyo hatuna. Mihemko na hamasa havitupeleki popote tujitathmini na tuanzishe shule za soka kwa watoto wetu wachezao soka bila mwongozo barabarani na viwanja visivyo rasmi. Soka la midomoni na matokeo yetu ya mfukoni havina nafasi katika weledi.
    Ama kwa kuwa ukweli hatuupendi iko misemo hii "tutamaliza sabuni, kaniki ni rangi yake... au tuendelee kusubiri embe chini ya mnazi"
    Vema tuendelee kujenga misingi ya soka toka awali ili tupate tija la sivyo MAUMIVU YATATUHUSU SANA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu kocha cjawah ckia CV ya timu alizofunfidha,Bali utasikia alicheza Barcelona,inasaidia non kucheza bsrca

      Delete
  4. Acheni hizo, vilaza nyie mbona Lesotho tulipocheza ano hapa nyumbani hatukuwafunga? na Samatha akiwemo. Si ajabu kufungwa huko Lesotho!

    ReplyDelete
  5. KOCHA AKAPUMZIKE TU KWAO HUKO, ATUACHIE TIMU YETU. UPANGAJI GANI ULE WA KIKOSI!

    ReplyDelete
  6. Kaona ameelemewa katikati na pia beki ina makosa mengi, bado kashindwa kufanya mabadiliko mapema. anakuja kutufanyia makusudi eti anabadilisha wachezaji dkk ya 92! Utamfunga nani wakati upo nyuma ya goli 1, si hata kama ni mimi nisiyejua kupanga kikosi, nawaambia wachezaji wote watande ndani ya 18. tuone kwa dakika hizo nane mtasazishia wapi. KOCHA UMETU - COST!! ARUDI KWAO HUYU.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic