November 21, 2018


Wakati kukiwa na sintofahamu ndani ya Yanga juu ya Mgombea nafasi ya uenyekiti, Mwanachama Lusajo Kisanda amewataka Yanga kujaza nafasi hiyo ili kuja kumshawishi Yusuf Manji aje awekeze ndani ya klabu.

Hatua hiyo imekuja kutokana na wanachama wengi wa klabu hiyo kutaka nafasi ya Uenyekiti isihusike katika uchaguzi wakiamini kuwa bado Yusuf Manji ni Mwenyekiti wao.

Kisanda ameeleza kuwa wao hawana namna tena zaidi ya kujaza nafasi yake kwa maagizo ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili baada ya hapo watajua namna ya kuja kumshawishi taratibu.

Mwanachama huyo anaamini kama Yanga ikifanya uchaguzi na kuja kuumaliza salama, kitakachofuata ni kufanya jitihada za kuzungumza na Manji ili awekeze ndani ya klabu.

Tayari zoezi la uchukuaji fomu kwa nafasi zote limefungwa juzi na kinachosubiriwa ni zoezi la kurejesha fomu hizo kisha mapingamizi na kampeni kushika hatamu baadaye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic