KARIA AWAKA JUU YA BARUA YA YANGA KUBADILI JINA, AAHIDI KUCHUKULIA WATU HATUA ZA KISHERIA
Na George Mganga
Baada ya barua kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusambaa ikieleza Yanga wanapaswa kubadilisha jina lao kutoka Young Africans Sports Club kwenda Young Africans Football Club, Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia, amesema awatachukulia hatua za kisheria walioweka mtandaoni.
Akizungumza mbashara na kituo cha Radio Clouds kupitia Sports Extra, Karia amesema hajajua ni nani ameiweka barua hiyo mtandaoni na atafanya kila jitihada za kumsaka mhusika ili amkamate.
"Nashangaa sijui ni nani aliyeipeleka barua hiyo mtandaoni, lazima nimtafute na nitamchukulia hatua za kisheria, lakini barua hiyo haijaandikwa kwa Yanga pekee bali ni kwa klabu zote ambazo zinatumia jina la Sports Club" alisema.
Licha ya kusambaa kwa barua hiyo, Karia amesema kuwa ni ya kweli na si kwamba imetumwa kwenda Yanga pekee bali ni kwa klabu zote zinazotumia jina la Sports Club badala ya Football Club.
Rais huyo amesema maagizo hayo yametolewa na Shirikisho la Soka duiani (FIFA) kutokana na jina Sports Club huwa linahusisha michezo mingine ambayo ni nje ya mpira wa miguu.
Barua hizo Karia ameeleza zimeshaandaliwa kwa timu zote husika ili kuondoa mkanganyiko wa kutumia jina hilo ambalo linaenda tofauti na klabu zenyewe hapa nchini kwani zinahusika na mpira wa miguu pekee.








😲😲😲😲😲😲😲😲😲
ReplyDeletekama maagizo yametoka fifa wangeanza na vilabu kama madrid maana wao wana timu za vikapu na michezo mingine ulimbukeni wa huyu kiongozi wa tfff ndio umatupaqtia sare lesotho
ReplyDelete