November 14, 2018



BAADA ya timu ya AS Kigali ya Rwanda kuyumba kifedha na kulazimika kuvunja mkataba wa straika wa zamani wa Simba, Elias Maguri kumesababisha aweze kutua timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC.

Maguri amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo akitokea kwenye soka la ushindani na sasa amerejea kwenye ligi ya nyumbani.

"Nafurahi kurejea kwenye ligi ya nyumbani, japo haikuwa malengo yangu kwa kuwa nilikuwa nahesabu za kucheza kimataifa, sina jinsi, nimesaini KMC nitapambana kuhakikisha nacheza kwa mafanikio kama ilivyokuwa ndoto yangu tangu naenda Oman," alisema.

Maguli amevunja mkataba wake na timu yake hiyo ya Rwanda kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni ukata ndani ya timu hiyo, aliwahi kuchezea pia Stand United.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic