November 28, 2018


Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, ameeleza kuwashangaa mashabiki waliokuwa wanaoponda kiwango cha mchezaji Heritier Makambo kutokana na kushindwa kuonesha kile wanachokihitaji.

Zahera ameibuka na kauli hiyo kutokana na lawama nyingi kutoka kwa mashabiki wa Yanga kuanza kuhoji juu ya usajili wa mchezaji huyo kuwa haukuzingatia matakwa ya timu.

Mkongomani huyo ambaye amekuwa hafichi la moyoni pale anapokuwa nalo, amefunguka hayo na kuwataka wanayanga ni vema wakawa na uvumilivu kwani ipo siku mambo yataenda sawa.

Aidha, Zahera amemtaja pia kipa Klaus Kindoki akisema anamjua vizuri pamoja na Makambo kuwa wanahitaji kupewa muda na anawaamini wachezaji hao watakuja kufabya vizuri.

Kindoki amemtetea pia juu ya lawama anazopewa na mashabiki wa Yanga akiamini kiwango chake ni kizuri na ipo siku atawaonesha makali yake uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic