November 7, 2018


Mshambuliaji wa timu ya Stand United, Alex Kitenge ambaye alikuwa wa kwanza kufunga 'Hat-Trick' msimu huu mbele ya Yanga amezidi kuandamwa na majanga ikiwa ni pamoja na ukame wa mabao  na kusumbuliwa na Malaria.


Kitenge tangu awafunge Yanga ameshindwa kufurukuta mbele ya timu nyingine licha ya kupata nafasi ya kucheza hali ambayo anasema inatokana na mabeki kumkamia akiwa uwanjani kwa kuwa wanamhofia.
 Kitenge amesema kuwa kwa sasa hali yake kiafya sio nzuri kwa kuwa anasumbuliwa na Malaria hivyo hana uhakika wa kuweza kucheza mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting.


"Kwa sasa sipo vizuri nasumbuliwa na Malaria, bado naendelea na dozi kwa kuwa nilienda hospitali nikapewa dawa hivyo sitaweza kuwa sehemu ya mchezo wa leo tusubiri kama hali itabadilika nikawa fiti kiafya," alisema.


Kutoka Championi

1 COMMENTS:

  1. xaxa kama mzee Akilimali alisema "Chirwa alipelekwa kwa Mganga "ili aanze kufunga magori, watashindwaje kumchawia huyo aliyewapiga hattick?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic