November 21, 2018





Baada ya Stars kushindwa kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Lesotho Jumapili iliyopita, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kocha wa Stars, Emmanuel Amunike aachwe afanye kazi yake.

 Stars ilipunguza matumaini ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani  nchini Cameroon baada ya kupoteza mechi hiyo kwa kupigwa bao 1-0.

Sasa Stars yenye pointi tano, inatakiwa kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Uganda na kuomba Mungu, Cape Verde waichape Lesotho.

Karia alisema kuwa anafahamu kuwa matokeo hayakuwafurahisha Watanzania wengi lakini pia wanapaswa kuheshimu  taaluma ya kocha.

“Kwanza naomba radhi kwa Watanzania kutokana na aina ya matokeo ambayo timu ilipata wajue ndiyo mpira una matokeo matatu, ninaamini ipo nafasi kwenye mechi ijayo.

 “ Lakini Watanzania wanapaswa kujua kila mtu ana majukumu yake, hivyo tuache kumuingilia mwalimu aachwa afanye kazi sababu anajua nini anafanya  na yeye ndiye alikuwa na wachezaji.

“ Hivyo tumpe nafasi mwalimu na tujue kuwa Stars imeenda kucheza na timu kubwa ya nchi na siyo ya wilaya kama watu ambavyo wanadhani.

 “Mimi sijavunjika moyo nipo pamoja na Rais Magufuli, tunaamini tutashinda mbele ya Uganda na suala lile la milioni 50, msimsemee kwa kuwa anajua mpira kuliko Watanzania wengi,”alisema Karia.

5 COMMENTS:

  1. Mimi nasema kuwa Taifa Stars haitaweza kuifunga Uganda Cranes

    ReplyDelete
  2. Amunike hata timu ikishinda dhidi ya Uganda bado hafai kuwa kocha was t.Stars.......kwangu Mimi kocha bora na ataendelea kuwa bora in Kim Paulsen tu

    ReplyDelete
  3. Kwahiyo hiyo mechi moja iliyobaki ndo haitakuwa na matokeo matatu? Itakuwa na matokeo mangapi PREZIDA WA TFF?. Msimtetee mtu hapa, mnaendelea kulivumilia jipu wakati limeshaiva hilo! hilo dawa yake ni kulitumbua tu ili watanzania tuweze kuepuka maumivu makubwa tutakayoweza kuyapata hapo baadae.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic