November 22, 2018


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa mbinu atakazotumia dhidi ya Lipuli FC, kesho uwanja wa Taifa ni tofauti na vile wanavyofikiria kwa kuwa hakuna anayeweza kukariri mipango yake.

Aussems amesema hakuna mwalimu ambaye anaingia uwanjani akifikiria kupoteza mchezo, kwa mbinu ambazo amewapa wachezaji ana uhakika wa kupata matokeo.


"Ushindani ni mkubwa, siwafikirii Lipuli FC peke yao, kuna timu nyingi ambazo zinashiriki ligi, nimewaambia wachezaji nahitaji matokeo ili kuweza kuendelea kuleta ushindani hasa kwa wakati.


"Kosa lao kubwa siku zote ni kutengeneza nafasi na kushindwa kuzitumia, hilo nimewaambia na nimewapa kazi ya kufanya wakiwa uwanjani, kila mchezaji ana jukumu lake," alisema Aussems.


Lipuli FC wamecheza michezo 13 na kujikusanyia pointi 12 huku Simba wakiwa wamecheza michezo 11 na kujikusanyia pointi 26.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic