November 7, 2018


Na Lunyamadzo Mlyuka

Baada ya kukubali kupoteza michezo miwili mfululizo, uongozi wa timu ya Ruvu Shooting umebainisha kinachowakwamisha kupata matokeo katika mechi zao na kuahidi kufanyia kazi ili kupata matokeo katika michezo inayofuata wakianza leo na Stand United.

Ruvu Shooting imepoteza pointi sita katika mechi zake mbili za hivi karibuni ambapo mchezo wa kwanza walicheza dhidi ya Simba wakafungwa mabao 5-0 na mchezo wa pili ulikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar walipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 hali iliyofanya uongozi kushtuka.


 Ofisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa kinachowasumbua wachezaji wake ni umakini wa kumalizia nafasi wanazotengeneza pindi wanapokuwa uwanjani wamekuwa wakifanya hivyo katika michezo yao hali inayowafanya wasipate matokeo.


"Matokeo tu ya mpira ambayo yanatukuta kwa sasa, wachezaji wanashindwa kumalizia nafasi ambazo wanazitengeneza wakiwa uwanjani hali ambayo inafanya tushindwe kupata matokeo ila hilo benchi la ufundi limeliona na linafanyia kazi tutaona matokeo yake katika mechi zetu zinazofuata.


"Kwa upande wa kiuchumi huko hatuna shida, tumemalizana na wachezaji wetu hasa kwa upande wa mishahara yao wote hatuna deni, pia wanakula vizuri wakiwa kambini tunawapa mpaka maziwa wanywe wawe na nguvu uwanjani," alisema.


 Leo Ruvu Shooting watacheza na Stand United katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani ikiwa ni mchezo wao wa 13, kwa michezo yao 12 waliyocheza wamefikisha pointi 13 ambazo zinawafanya wawe nafasi ya 12.

1 COMMENTS:

  1. Hivi masau bwire ni kocha? Ruvu shooting haina kocha? maana kila kitu masau bwire mambo mengine anazidisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic