November 24, 2018

Alhamdulillah nimepata fursa ya kuanza kusoma nje ya Taifa langu ninalolipenda sana,kisha nikaja nyumbani, nimetembea nchi zaidi ya Hamsini kote ulimwenguni, kuanzia Europe hadi Asia ambapo pia nilibahatika kujiongezea maarifa ya kielimu kule China,na nimetembea pia nchi kadhaa za kiafrika ila ni Tanzania pekee ndio nimewahi kunyanyaswa kisa ualbino wangu.

Tanzania ndiyo nchi pekee unaweza kupita mtaani mtu akakuita zeruzeru huyo, ndio taifa pekee wakati nagombea CCM uenezi nilidhihakiwa nisichaguliwe kisa zeruzeru,ndio Taifa pekee linalochinja na kuua watu kwa uzeruzeru wao!ndio taifa pekee mtu anakuita zeruzeru mitandaoni na asiguswe na mamlaka!!

Inasikitisha sana kuona Yanga na Simba ambao ni jadi na jadi kutaniana, watu kuniita kwa uzeruzeru wangu! Mimi na huyo mtoto na walemavu wote hatukuomba!! 

Ni matakwa ya Allah mwenyewe!! Na kinachoniuma wengi wanaotusi ni waislaam kwa majina yao,kisha utakuta aliyetukana kaandika status Mungu ndio muweza!! Hv hujui waweza kuwa mlemavu wa kesho?

Rais wangu najua dhamira yako njema kwetu ila naomba uwaambie TCRA wasimamie hili!!
Mpira ni utani na furaha sio matusi yaliyojaa kufuru!! Hivi hamjiulizi why kuna mambo hayaendi Tanzania.

Okey mm nitabaki nilivyo na maisha yangu c haba,ila nawafikiria wenzangu wengine!! Naipenda nchi hii ila sio siri ndio taifa la ajabu zaidi duniani kwa watu wake kuchinja,kutukana,kukebehi na kuwadhihaki Watu walemavu.

Niliwahi kukataliwa kwenye Radio moja kuajiriwa kisa Zeruzeru,nawashukuru sana Simba Sc kwa kuona talent na uwezo wangu kisha kunipa fursa ambayo hakuna mtanzania atadoubt!! Okey endeleeni kututusi mliobarikiwa viungo kamili🙏

24 COMMENTS:

  1. dah.la ilaha illa anta.inni kuntu mina dhalimiin.ndio maana kuna kila kitu na vingine havipo popote.lkn tumekosa Baraka kwa tabia zetu.mimi ni adui mkubwa wa watu hao hata awe nani kwangu.kukashifu maumbile ni kufuru.najua mioyo yao inaungua kwa ujumbe huo.

    ReplyDelete
  2. kaka umeongea vizuri sana tatizo watanzania elimu ya kumjua mungu na qadari zake wengi wao hawana...hata Mimi nachukizwa sana na vitendo vya kibaguzi serikali nafikiri imesikia.

    ReplyDelete
  3. mkubwa hilo suala inabidi likomeshwe kwa nguvu zote mpira furaha salehe umesikia malalamiko ya mkubwa tumia ukurasa wako kukemea hilo

    ReplyDelete
  4. Sina hakika kwakuwa nipo mbali na nyumbani kipindi lakini nadhani baada ya udanganjifu katika makanikia ya dhahabu serikali iliunda tume ya kuchunguza wizi ule na kufuatia utungwaji wa sheria maalum ya kuhakikisha Serikali inadhibiti mapato ya maliasili madini. Sasa baada ya mauaji na unyanyasaji wa watu wenye umemavu wa ngozi kushamiri nchini sidhani kama kuliundwa tume maalum ya kuchunguza kwa kina aina hii ya unyama wa kijinga. Na kama kuliundwa tume basi sijawahi kusikia bunge likijadili na kutunga mswaada maalum wa kuwalinda maalbino na matendo ya unyanyasaji. Kwangu mimi sioni tofauti ya albino na mtu mwengine sijui hao watu wenye mawazo tofauti kuhusu muonekano wa albino laana hiyo wameipata wapi? Unamsimanga au kumkejeli albino kwa kipi kibaya alichonacho? Kuna mengi ya hovyo hufanyika katika jamii ya kitanzania lakini bado na jivunia utanzania wangu ila kama kuna jambo natamani nisingekuwa mtanzania basi ni hili la ukatili juu ya maalbino. Yaani hili suala linatakiwa kukomeshwa na kukemewa kwa nguvu zote.

    ReplyDelete
  5. Haki ya mungu imeniuma jamani kaandika kwa uchungu sana daaa..!!!

    ReplyDelete
  6. Tatizo la Haji ni kashfa anazokuwa nazo kwa wapinzani wake na maneno machafu!! Ndo sababu kubwa ya kudhalilishwa, mbona wapo albino wengine na wana maisha ya kawaida wala hueaoni kutukanwa mitandaoni!? Kabla ya kulalamika, hebu jiangalie wewe kwanza unaishije na jamii iliyokuzunguka!? Usemaji sio kashfa, unaweza kuongea vizuri tu bado ukawa msemaji. Dismas au msemaji wa Azam ni mfano wa kuigwa. Other wise ukijua kunawia mbele, kuna watu wanajua kunawia nyuma

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uko sahihi Nanara ni mdhalilishaji na msema ovyo kupitia nafas yake ya usemaji SSC. Abadilike na yeye badala ya kulalamika tu...

      Delete
  7. Manara huwa unaongea maneno mabaya xna Mara nyingne sasa watu wengine wanapata hacra na kukuita ivyo c vizur kukuita ivyo ila na wewe jiangalie unakumbuka ulivyowadhihak wale Wa wadada mabonge kwenye tangazo la Yanga ..........Anza wewe kutumia lugha nzur ht kama ni utan usitumie lugha ya kashfa Kwa binadam wenzako

    ReplyDelete
  8. Enter your comment...Ni kweli hili suala hata mimi limekuwa likinikwaza hasa kwa mashabiki wa yanga utani ni sehemu ya maisha lakini inafikia wakati wanampost Haji manara na kumkebehi kwa ulemavu wake wa ngozi hivi najiuliza kuwa hawa nao hawajuikuwa kabla haujafa haujaumbika? kwa ufupi Haji Manara hakupenda kuwa vile na pia manara hana tofauti na sisi kwan anafanya kazi zake kama binadamu wa kawaida na kuwazidi wenye kujiringingia ngozi zao
    manara mungu akulinde ipo siku watapata majibu hapahapa duniani

    ReplyDelete
  9. Haji Manara, atafute kitu kingine cha kukishabikia na kukisemea kwa staili yake sio soka.

    Tena soka la Tanzania lililojipanga kwenye Yanga/Simba.yy yuko Simba ili apate raha lazima awakejeli Yanga katika jambo lolote lile.

    Na yy ajiandae kujibiwa katika hali yoyote ile lkn itafsiriwe kuwa si ubaguzi ni UTANI.

    Tshitshimbi alipotua nchini na kupiga Mpira mwingi akiwakusanya viungo Wa Simba wapenzi Wa Yanga wakafurahi licha ya kufungwa kwa penalti vicheko havikuwaisha.

    Simba kujibu mapigo wakamuita Tshitshimbi kuwa ni SHISHI BABY wakimfananisha na muimbaji Wa kike Wa bongo flavour.

    Haji Manara msemaji Wa klabu hakuliona hili kama ni udhalilishaji ,ubaguzi na sio UTANI.

    SHISHI BABY mwenyewe alisema haoni tatizo kwani anaamini halikutumika kwa maana mbaya.

    Haji Manara akajitokeza na kulishabikia suala hili, aliposhambuliwa mtandaoni akajitokeza na kusema hakuwa na nia mbaya ila alishangaa SHISHI baby kukubali jina la kike litumiwe na Mwanaume.

    Nimemfuatilia sana Haji Manara hapendi kuwa chini, kuzidiwa maneno, daima anapenda awe juu, asikike yeye tu.

    Sasa ukiona anakimbilia kushtaki kwa jamii na kwa Mungu ujue kazidiwa.

    Kumbukeni mtoto Wa kichaga alivyokuwa anampopoa bila kumtaja ngozi huku timu yake ikiwa hoi uwanjani.

    Alikuwa akilalamika na kuitaka Tff imuadhibu Muro.

    Hivi nn maana ya MITULINGA alivyolitumia HAJI , jibu kwake ingepaswa ajibiwe nn ? Lkn alijibiwa nn?

    Alichojibiwa kwa ustaarabu bado akaendeleza malumbano kwa maana jibu alilopewa aliona halifanani na alichotaka.

    Lugha ya Mpira tafsiri zake ni utani, ukiona unazipeleka Police,TCRA au mamlaka zingine za adhabu ujue umechoka tafuta sehemu nyingine.

    ReplyDelete
  10. Haji Manara, atafute kitu kingine cha kukishabikia na kukisemea kwa staili yake sio soka.

  11. Haji Manara, atafute kitu kingine cha kukishabikia na kukisemea kwa staili yake sio soka.

  12. Ukisoma baadhi ya maoni hapo juu utaona yakuwa watu wanatafuta kisingizio cha utani wa mpira ili kuleta madharau juu ya maumbile ya mtu. Kuna uhusiano gani kati ya utani wa mpira na kwenda kumkutukana mtu jinsi amivyoumbwa? Ukiachana na Manara ambae washenzi wanaomfanyia dhihaka kwa kisingizio cha mpira vipi hao maalbino wengine tena watoto wadogo wanaouwawa au kujeruhiwa kosa lao ni nini?

    ReplyDelete
  13. With all due respect naomba nipingane na Haji Manara...
    Kwanza kabisa watu watambue Haji ni mtu asiyependa kuzidiwa kimaneno anataka always awe juu
    Haji anapolalamika baadhi ya mashabiki kumtukana kwa jinsi alivyo kwanza ajiulize haya
    1.Sio Manara huyu aliyewadhihaki wale wadada mabonge wa Yanga bila kujali hisia zao juu ya ile dhihaka
    2.Simba walipoamua kumuita Tshishimbi 'Shishi Baby' sio Manara huyu ambaye baada ya kukemea hiko kitu aka support tena kwa kebehi na dhihaka,wanaume menzangu kuna feeling mbaya ambazo mwanaume huzipata kama pale anapofananishwa na mwanamke? Manara hakujali hili.
    Kwa hiyo kimsingi kabla ya kuwalaumu wanaokudhihaki jiangalie kwanza wewe ni msafi?
    Simba na Yanga zote zina wasemaji kwa nini hujifunzi kutoka kwao?,wewe Redioni unaacha kufanya kazi ya Usemaji unaleta ushabiki huku ukijua huwezi kudeal na consequences za kuwa mshabiki.
    Simba na Yanga ni kebehi,dhihaka,matani,matusi ambayo havitakaa viishe hadi dunia inafikia mwisho.Ukijiona huviwezi jifunze kuwa kama wasemaji wa Yanga na Azam.

    ReplyDelete
  14. Haji Manara maneno uliyosema yametutia uchungu sote hata tunaoshabikia Yanga ila nimesikitishwa pale ulipotumia neno WAISLAM ndio wanaokusema zaidi kwa vile tu majina yao ni ya Kiislam !!! Jaribu kutoingiza mambo ya dini katika masaala binafsi maana dini zote zinawatetea binaadam wa aina zote na anapokosea mtu isiingizwe dini yake maana haikumtuma kufanya hivyo!!

    ReplyDelete
  15. Akitaka asitaniwe basi naye ajitathmini ktk maneno yake.yeye kama msemaji wa simba aache kuwa msemaji wa yanga.

    ReplyDelete
  16. Akitaka asitaniwe basi naye ajitathmini ktk maneno yake.yeye kama msemaji wa simba aache kuwa msemaji wa yanga.

    ReplyDelete
  17. Akitaka asitaniwe basi naye ajitathmini ktk maneno yake.yeye kama msemaji wa simba aache kuwa msemaji wa yanga.

    ReplyDelete
  18. Akitaka asitaniwe basi naye ajitathmini ktk maneno yake.yeye kama msemaji wa simba aache kuwa msemaji wa yanga.

    ReplyDelete
  19. Ni ulimbuken tu wa waafrica hasa ambao n ignorant, so vumilia mkubwa mungu anamakusud yake kuwa ulivyo, nawatajibiwa saw a na kauli zao mbovu!!! Binafsi nakuelewa Mtan wangu!!!! Pole sanaaa mkubwa!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic