Taarifa za kuhitajika kwa beki huyo ambaye ni tegemo katika kikosi cha Mtibwa kwenda Yanga zimeanza kushika kasi haswa kipindi cha dirisha dogo kufunguliwa.
Kwa mujibu wa Idara ya Habari kutoka Yanga, imeeleza kuwa wao hawana mazungumzo yoyote na Rodger kwani wanafuata mahitaji ya benchi la ufundi.
Idara hiyo imesema usajili wote unaofanyika Yanga si wa ilimradi tu bali huwa wanasubiri taarifa kutoka benchi la ufundi na kisha Kamati ya Usajili huwajibika.
Licha ya kuenea kwa tetesi hizo, Mtibwa Sugar nao wameeleza kuwa ni taarifa za vijiweni tu wala hazina ukweli wowote.
Kupitia Msemaji wa timu hiyo, Thobias Kifaru, amesema wao hawana taarifa hizo na wala hawajazungumza na Yanga huku akisema pindi kipindi cha usajili kinapofika tetesi kama hizi huwa ni za kawaida.








0 COMMENTS:
Post a Comment