JUMLA ya magari 12 yalibeba mashabiki kutoka Tanzania na wale ambao wanaoishi nchi jirani na Lesotho yameanza safari mudaa kuelekea kwenye Uwanja wa Setsoto hapa Maseru, Lesotho.
Mashabiki ambao wametumia usafiri wa basi na wengi wakitumia gari zao binafsi kwa pamoja wanaelekea kwenye Uwanja huo tayari kuishangilia Stars itakayocheza kwenye Uwanja huo dhidi ya wenyeji Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Africa 'Afcon' mwakani.
Stars inashuka kwenye mchezo huo ikiwa inahitaji ushindi ili weze kufuzu kutoka Kundi L baada ya jana Uganda kufanikiw kufuzu kufuatia kufikisha pointi 13 baada kuifunga bao 1-0 Cape Verde.
Mbali ya mashabiki hao katika msafara huo wapo viongozi wa baadhi ya klabu za Ligi Kuu Bara akiwemo aliyekuwa kaimu rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Gain' na msemaji wa timu hiyo, Haji Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment